MAZOEZI YA IMANI

MAZOEZI YA IMANI
MAZOEZI YA IMANI,SOTE TUSHIRIKI KATIKA MAZOEZI YA SALA

Sunday, November 20, 2011

Muasisi wa dhehebu la misa ya pili afungwa


  

Na Mwandishi maalum.Pichani ni askofu wa kanisa Anglikana Dayosisi ya Ruvuma mhashamu Dk.Maternus Kapinga akitoa maoni yake kuhusu kufungwa kwa aliyekuwa kiongozi wa kuvuruga kanisa
  

MUASISI na kiongozi wa wakristo wa dhehebu la misa ya pili  wilayani Mbinga mkoani Ruvuma Joseph Lombola amehukumiwa kifungo cha miezi 12 kwa kosa la kufanya vurugu katika kanisa la Anglikana la Kristo Mfalme mjini Mbinga.

Lombola ambaye pia ni katibu wa Tume ya Utumishi ya Walimu (TSD) wilayani Mbinga ametiwa hatiani pamoja na  Martin Mawala aliyeachishwa upadre wa kanisa Anglikana kwa kutomtii Askofu wa Dayosisi ya Ruvuma.
Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Mbinga Frank Mahimbali akitoa hukumu alisema ameridhika na upande wa mashitaka kuwa washitakiwa bila uhalali walifanya vurugu wakati ibada ikiendeshwa na padre  Andrew Nkomola wa kanisa la Kristo Mfalme mjini Mbinga.
Kutokana na hali hiyo ,mahakama iliwatia hatiani hivi karibuni na kuwahukumu kifungo cha nje  cha miezi 12 kila mmoja na kwamba katika kipindi hicho  hawatakiwi kufanya kosa la aina yoyote.
Awali mwendesha mashtaka wa polisi Inspekta Isaya alidai washitakiwa  hao walitenda makosa hayo Agosti 16 ,2009 katika kanisa hilo ambapo washitakiwa waliingia kanisani na kwenda madhabahuni kisha waliondoa vitambaa,kutupa vitabu  vitakatifu na sakramenti takatifu jambo ambalo lilisababisha vurugu kutoka kwa waumini.
Habari   zaidi kutoka ndani ya kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma zinadai kuwa  Lombola ambaye hivi sasa anatumikia kifungo cha mwaka mmoja ndiye kiongozi wa kikundi cha kidini  kinachojiita Wakristo wa Misa ya Pili(SECT) ambacho kinaendesha shughuli zake mkoani Ruvuma bila uhalali wa kuwepo kisheria kwa kuwa hakina usajiri wowote.
 Askofu wa kanisa Anglikana Dayosisi ya Ruvuma Dk.Maternus Kapinga  amesema amani ya kanisa hilo itaimarika zaidi baada ya kufungwa kwa muasisi wa SECT  ambaye alikuwa ni muhimili wa kikundi  cha Wakristo wa Misa ya Pili  ambao kazi yao kubwa ni  kulaghai,kuposha,kuharibu kanisa la Mungu na kuvuruga uongozi wa Askofu wa Ruvuma.
Kwa mujibu wa Askofu Kapinga waasisi,viongozi na wafadhili wakuu wa SECT ni wanasiasa,watu walioshindwa huduma takatifu  na watu wanaowania vyeo na mali katika kanisa hilo ambao wamejiengua kutoka katika kanisa hilo kwa madai  ya kutotaka kumtii Askofu wa Ruvuma wa awamu ya tatu.
  
“Lengo kuu la kikundi hicho ni kumwaga damu isiyo na hatia hasa wakidhamiria kumuondoa Askofu wa Ruvuma kutoka huduma takatifu aliyoitiwa na Mungu,mbinu kuu ambayo wanaitumia ili kutekeleza lengo hilo ni kupotosha na kutowaambia watu ukweli’’,alisema mkristo  ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini.
Mkristo huyo anabainisha zaidi kuwa kikundi hicho kinawashawishi watu wawafuate katika kumkataa Askofu wa Ruvuma na kwamba walifanikiwa kuanzisha vikundi katika maeneo ya Mbinga,Songea,Chiulu,Liuli na Puulu, vikundi ambavyo hivi sasa vyote vimekufa na wakristo wametubu na wamerudi kwa Askofu wa kanisa la Mungu.
Viongozi wa SECT ili kutimiza azima yao ya kulivuruga kanisa ,waliamua kuwaajiri makasisi waliosimamishwa ili wawe viongozi wao wa kiroho.Makasisi hao walisimamishwa kutoa huduma takatifu katika kanisa hilo baada ya kufanya makosa mabaya yakiwemo kuvunja ndoa, kutokutii mamlaka ya Mungu na kuishi na  vimada.
Askofu Dk.Kapinga anasema waumini wa dhehebu la Misa ya Pili   wamekuwa wakiigiza ibada zao kanisani na kwamba lengo lao halikuwa kumuabudu Mungu bali ni kuleta fujo ili ulimwengu useme Dayosisi ya Ruvuma ni yenye ni migogoro.
“Watu waliozuiwa kutoa huduma ya ukasisi katika kanisa hilo ,walikaidi amri hii ya Mungu na mamlaka halali ya kanisa,watu hao wakijua kuwa hawana mamlaka ya kasisi,lakini waliwadanganya watu  na serikali kwa kuwaibia malipo,mathalani kwa kufungisha ndoa bila kulipia kibali cha kufungisha ndoa’’,alifafanua Askofu Dk.Kapinga.
Kikundi cha  cha dhehebu la Misa ya pili kilijitokeza hadharani Desemba mwaka 2007  na hadi mwaka 2010 kikundi hicho kilikuwa kimemalizika na Dayosisi  ya Ruvuma kuwa katika hali ya amani na utulivu kutokana na juhudi zilizozaa matunda kwa ushirikiano baina ya waumini,uongozi wa kanisa  na viongozi wa serikali katika ngazi mbalimbali mkoani Ruvuma.
Takwimu  toka ofisi ya Askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma zinaonesha kuwa hadi kufikia Oktoba 31  mwaka huu kanisa hilo lina jumla ya waumini 41,000 ambapo dhehebu la Misa ya Pili lina waumini wasiozidi 50(hamsini).
Makala hii kwa hisani ya kanisa Anglikana Dayosisi ya RuvumaFriday, July 15, 2011

Zifahamu Dinari za Dayosisi ya kanisa Anglikana Ruvuma


Dinari za kanisa Anglikana Ruvuma pamoja na wachungaji wake hizi hapa

1.             Dinari ya Chiwindi Rural Dean
Fr. Bonaventula Mtaileni
Simu 0769 358777
Makao Makuu – Ng’ombo

2.             Dinari ya Ruhekehi:
Can Caswel Makita
Simu 0756 713118
Makao Makuu MbambaBay

3.             Dinari ya Jubilei        Rev. Fr. Benson Mpangala
Simu 0756-696163
Makao Makuu: Lundo

4.             Dinari ya Johnson     Rev. Fr. Luka Chihwalo
Simu 0765-959098
Makao Makuu: Liuli

5.             Dinari ya Watoto wasio na hatia
Rev. Canan Mashack
Ndunguru (Kaimu)
Makao Makuu: Mkili

6.             Dinari ya Mariamu Mbarikiwa Mama wa Mungu (MMMM)
Rev. Can AMOS Katambala
Simu 0763-433278
Makao Makuu: Ndongosi

7.             Dinari ya Nyota ya Bahari (Stella Maris)
Rev. Can Amos Katambala
Simu 0763-433278
Makao Makuu: Ndongosi

8.             Dinari ya Kusto Bambo
Rev. Fr. Andrew Mkomola
Simu: 0768-116753
M/Makuu: Mbinga

9.             Dinari ya Mashahidi wa Afrika
Rev. Fr. Philip Ngongi
Simu 0755-472954
MM: Songea

10.         Dinari ya Kristo Mshindi
Rev. Fr. Simon Ntauchila
Simu 0757-327291
M/M Namtumbo

11.         Dinari ya Kristo Mtawala
Rev. Fr. Ernest Mliwa
Simu 0768-448359
M/M Ruhimba 
IMETOLEWA NA UONGOZI WA KANISA ANGLIKANA DAYOSISI YA RUVUMA.

Watambue viongozi wa kanisa Anglikana Dayosisi ya Ruvuma
Askofu wa Dayosisi ni mhashamu Rt Rev. Dr Maternus K. Kapinga
                        P.O. BOX 135
                        Songea
                        Fax No. 025 2600100
                        Simu ya Mkononi: 0768 360580
            Barua pepe: Maternask@gmail.com


                       
 
 
VICAR GENERAL WA DAYOSISI
Rev. Can Kalistus B. Komba

 SLP.135 Songea
Simu ya mkononi: 0762 726534
 Barua pepe: revkkomba@yahoo.com
Katibu wa Dayosisi
                        Rev. Canon Caswel Makita
                        P.O. Box 1357
                        Songea
                        Simu ya mkononi 0756 713 118

Dean wa Kanisa Kuu (Cathedral) la Dayosisi
                        Rev. Fr. Erast Haule
                        P.O. BOX 1357
                        Songea
            Barua pepe: erasto. Haule@yahoo.com

MAHASIBU MKUU WA DAYOSISI
                        Rev. Fr. John George Mapunda
                        P.O. Box  1357
                        Songea
                        Simu: 0768-360583
            Email: revmapunda@hotmail.com

IDARA MBALIMBALI DAYOSISINI

IDARA YA UINJILISHAJI – KANDA YA MILIMANI
                        Rev. Fr. Denis Hyera
                        P. O. Box 1357
                        SONGEA
                        SIMU No. 0753-068011

IDARA YA UINJILISHAJI MWAMBAO WA ZIWA NYASA
                        Ev. Bartholomayo John Kaole
                        P.O. Box 1357
                        SONGEA
                       Simu: 0765-708520
IDARA YA AFYA

  KAIMU MGANGA MKUU WA HOSPITALI YA MTAKATIFU ANNA
    Dr. Denis Mahinya
    P. O. Box 1357
    SONGEA
     SIMU No. 0755-718855
       0712-813506
        Barua pepe

IDARA YA MAENDELEO
                        Rev. Fr. Erasto Haule

                     SLP 135   SONGEA.
                        Simu No. 0753-724988

KURUGENZI YA VIJANA KANDA YA MILIMANI
                        Rev. Fr. Simon Ntauchila
                        P.O. BOX 1357
                        SONGEA
                        Simu No. 0757-327291

KURUGENZI YA VIAJANA KANDA YA MWAMBAO WA ZIWA NYASA
                        Shemasi Barnaba Katambala
                        P.O. Box 1357
                        SONGEA
                        Simu No. 0753-722676

IDARA YA UMAKI
    Katibu wa Umaki: Mrs. Joyce Salimu
    P.O. Box 1357
   SONGEA
    Simu

KURUGENZI YA ELIMU NA MAFUNZO
                        Rev. Can Kalistus Komba
                        P.O. Box 1357
                        SONGEA
                        Simu No.0762-726534
          Barua pepe revkomba@yahoo.com
 Imetolewa na uongozi wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma.

Friday, June 3, 2011

Askofu Kapinga awapongeza waumini wake


Pichani ni Mhashamu Askofu wa kanisa Anglikana Dayosisi ya Ruvuma Dk.Maternus Kapinga
Na Mwandishi maalum.
 Askofu  wa kanisa Anglikana Dayosisi ya Ruvuma Dk.Maternus Kapinga amewashukuru waumini wa kanisa kuu la mtakatifu Nicholous ambalo anasema siku zote limesimama imara katika kutetea haki za kanisa hilo dhidi ya maadui wachache ambao kwa makusudi walitaka kuliingiza kanisa hilo katika migogoro na kuhatarisha amani ya kanisa la Mungu.

Dr.Kapinga alibainisha kuwa katika kipindi chake cha uongozi katika Dayosisi hiyo amekumbana na mafanikio makubwa ya kimwili na kiroho kwa waumini licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zilitokana na waumini wachache  ambao walipania kuuangusha uongozi halali  wa kanisa hilo.

“Mwaka 2010 ulikuwa na matukio ya ajabu kwa kanisa likiwepo tukio la Machi,30,2010 ambapo maadui wa kanisa la Anglikana kwa kufadhiliwa  walipanga kuuangusha uaskofu wangu kutokana na nguvu ya fedha walifanikiwa kuteka kila kitu,lakini walisahau kuwa uaskofu wangu nimewekwa na Mungu,mpango wao ukashindikana na ngome ya mwisho ya maadui wa kanisa  imeanguka huko Chiulu Nyasa na hivi sasa kanisa katika Dayosisi nzima ya Ruvuma ni jeupe,lenye upendo na amani”,anasisitiza.

Wakati huo huo Dk. Kapinga  ameikumbusha serikali kuendelea kusisitiza amani,upendo na umoja kwa watanzania ili Taifa liendelee  kuwa kisiwa cha utulivu na kutoa rai kwa serikali kuanzia ngazi ya kijiji,kata,tarafa,wilaya,mkoa hadi Taifa  kuendeleza mitazamo aliyoiacha Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere siku zote kuhubiri amani,upendo na utulivu hali ambayo alisema imeifanya nchi kuendelea kuwa kisiwa cha amani.


Picha inawaonesha baadhi ya waumini wa kanisa la Anglikana la Msalaba Liuli wakifuatilia ibada kwa makini.

Hata hivyo kwa namna ya pekee Askofu Dr.Kapinga ameipongeza serikali ya mkoa wa Ruvuma kuanzia ngazi ya kijiji,kata,tarafa,wilaya na mkoa kwa  ushirikiano mkubwa ambao wameutoa katika kanisa la Anglikana hali ambayo imeleta amani kubwa miongoni mwa waumini wa kanisa hilo na kusisitiza kuwa serikali  imefanya kazi ya kuleta amani alioagiza Mungu moja kwa moja.
Askofu Kapinga akiwa katika kazi ya kichungaji

Friday, May 27, 2011

Karibu katika tovuti ya kanisa Anglikana Dayosisi ya Ruvuma

Picha hapa ni Askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma mshamu Dk.Maternus Kapinga akiwa katika moja ya shughuli za kichungaji katika kanisa la Mateka mjini Songea mara baada ya kutoa kipaimara kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mateka wakiwa pamoja na wazazi wao wote wakiwa na sura za furaha

Hapa Askofu Maternus Kapinga akitoa kipaimara kwa mmoja wa wanafunzi mjini Songea,wanaonekana kwa pembeni ni wasaidizi wake ambao kwa pamoja wakishiriki katika huduma ya kiroho.