Na Mwandishi maalum.
Askofu wa kanisa Anglikana Dayosisi ya Ruvuma Dk.Maternus Kapinga amewashukuru waumini wa kanisa kuu la mtakatifu Nicholous ambalo anasema siku zote limesimama imara katika kutetea haki za kanisa hilo dhidi ya maadui wachache ambao kwa makusudi walitaka kuliingiza kanisa hilo katika migogoro na kuhatarisha amani ya kanisa la Mungu.
Dr.Kapinga alibainisha kuwa katika kipindi chake cha uongozi katika Dayosisi hiyo amekumbana na mafanikio makubwa ya kimwili na kiroho kwa waumini licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zilitokana na waumini wachache ambao walipania kuuangusha uongozi halali wa kanisa hilo.
“Mwaka 2010 ulikuwa na matukio ya ajabu kwa kanisa likiwepo tukio la Machi,30,2010 ambapo maadui wa kanisa la Anglikana kwa kufadhiliwa walipanga kuuangusha uaskofu wangu kutokana na nguvu ya fedha walifanikiwa kuteka kila kitu,lakini walisahau kuwa uaskofu wangu nimewekwa na Mungu,mpango wao ukashindikana na ngome ya mwisho ya maadui wa kanisa imeanguka huko Chiulu Nyasa na hivi sasa kanisa katika Dayosisi nzima ya Ruvuma ni jeupe,lenye upendo na amani”,anasisitiza.
Wakati huo huo Dk. Kapinga ameikumbusha serikali kuendelea kusisitiza amani,upendo na umoja kwa watanzania ili Taifa liendelee kuwa kisiwa cha utulivu na kutoa rai kwa serikali kuanzia ngazi ya kijiji,kata,tarafa,wilaya,mkoa hadi Taifa kuendeleza mitazamo aliyoiacha Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere siku zote kuhubiri amani,upendo na utulivu hali ambayo alisema imeifanya nchi kuendelea kuwa kisiwa cha amani.
Picha inawaonesha baadhi ya waumini wa kanisa la Anglikana la Msalaba Liuli wakifuatilia ibada kwa makini.
Hata hivyo kwa namna ya pekee Askofu Dr.Kapinga ameipongeza serikali ya mkoa wa Ruvuma kuanzia ngazi ya kijiji,kata,tarafa,wilaya na mkoa kwa ushirikiano mkubwa ambao wameutoa katika kanisa la Anglikana hali ambayo imeleta amani kubwa miongoni mwa waumini wa kanisa hilo na kusisitiza kuwa serikali imefanya kazi ya kuleta amani alioagiza Mungu moja kwa moja.
No comments:
Post a Comment